BAKHRESA: MTU WA PILI KWA UTAJIRI AFRIKA MASHARIKIMfanyabishara mkubwa wa Kitanzania, Said Salim Bakhresa ndiye mtu wa pili kwa utajiri mkubwa Afrika Mashariki, akiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya $520 millioni (Sh832 billioni). Bwana  Bakhresa, ambaye himaya ya biashara yake imeenea katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, yuko katika nafasi ya 30 kati ya 40 barani Afrika.

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 63, anapata faida katika biashara za usagaji wa nafaka, vinywaji laini, usindikaji, usafiri wa majini na biashara ya mafuta. Kapuni yake ya Bakhresa Group huzalisha bidhaa zenye nembo maarufu ya Azam.

Orodha hiyo ya kila mwaka hutolewa na jarida maarufu la Kimarekani la Forbes Magazine na ilitolewa jana.

“Mauzo ya bidhaa za Bakhresa Group ni $800 millioni (Sh1.3 billioni) na kampuni hiyo ndio mzalishaji mkubwa zaidi wa unga wa ngano katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa na uwezo wa kila siku wa kuzalisha tani za ujazo 3,200,” jarida hilo limeripoti.

Majasiliamali mwenye utajiri kuliko wote Afrika Mashariki ni mfanyabiashara wa Uganda, Sudhir Ruparelia mwenye utajiri wenye thamani ya $900 millioni. Ni mtu wa 18 kwa utajiri barani Afrika. Mjasiliamali huyo mwenye umri wa miaka 56 anayeishi mjini Kampala anafaidika katika biashara za mabenki, mali zisizohamishika na hoteli.

Mtu wa tatu kwa utajiri katika ukanda huu ni Mkenya, Naushad Merali, akiwa na utajiri wenye thamani ya $410 millioni.

Wanigeria, Waafrika ya Kusini na Wamisri wametawala orodha ya watu kumi wenye utajiri zaidi barani Afrika, huku Aliko Dangote wa Nigeria akishika nafasi ya kwanza Afrika akiwa na utajiri wenye thamani ya $12 billioni.

Watu wengine katika watu hao kumi ni pamoja na Nicky Oppenheimer & family, Johann Rupert &family, Christottel Wiese na Patrice Motsepe—wote wakiwa wanatoka Afrika Kusini. Wengine ni  Mohamed Mansour, Naguib Sawiris na Nassef Sawiris kutoka Misri, Mike Adenuga kutoka Nigeria na Othman Benjelloun kutoka Morrocco.

Inasemekana kuwa Bw. Bakhresa alikuwa na maisha magumu wakati wa ujana wake. Jarida hilo linasema: “Mtu tajiri zaidi nchini Tanzania, Said Salim Bakhresa, aliacha kusoma akiwa na umri wa miaka 14 na kwenda kuuza viazi (chips), kisha akafungua mgahawa mdogo na hatimaye akaingia katika biashara ya usagaji wa nafaka. Leo hii, Kampuni yake ya Bakhresa Group imewaajiri zaidi ya watu 2,000 na ndio kampuni kubwa zaidi inayozalisha bidhaa za chakula nchini Tanzania.”
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.