ALAMA ZA UFAULU KIDATO CHA IV KUBADILIKA
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatarajia kubadili alama za ufaulu kwa wanafunzi wa kidato cha Nne ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi wanaomaliza kidato hicho kuingia Kidato cha Tano.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amesema Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa wanafunzi wengi wanaomaliza kidato cha Nne wanashindwa kuendelea na masomo ya kidato cha Tano licha ya kuwa na uwezo mzuri wa kitaaluma.

Mulugo ametoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na Star Tv kabla ya kuufunga mkutano wa mwaka wa Wamiliki wa Shule za Sekondari na Vyuo Binafsi Tanzania, TAMONGSCO, jijini Mbeya.
Baada ya mazungumzo haya, Mulugo, anakwenda kuzungumza na wajumbe wa mkutano huo na kupata fursa ya kubainisha sababu za kuifikia hatua hiyo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa TAMONGSCO Taifa, Mahmoud Mringo, baadhi ya maagizo yanayotolewa na Serikali katika uendeshaji wa elimu nchini ni kikwazo cha maendeleo ya sekta hiyo.

Baadhi ya wamiliki wa shule, wanasema umefika wakati kwa Serikali kutoa ruzuku mashuleni.
Mkutano huo wa siku mbili uliowahusisha wamiliki wa shule na vyuo binafsi kutoka mikoa yote nchini umeakisi changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini ili kuboresha sekta hiyo.

CHANZO: STAR TV
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.