AL-SHABAAB: MAKUBWA ZAIDI YANAKUJALicha ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kutangaza ushindi dhidi ya watekaji wa jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi, wapiganaji wa al-shabaab wamesisitiza kuwa wataendelea kupambana.

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Aljazeera, msemaji wa operesheni za kijeshi wa kundi hilo, Sheikh Abdulaziz Abu Muscab, alimtaka Rais Kenyatta kuyaondoa majeshi yake nchini Somalia, la sivyo mashambulizi mengine ya kigaidi yapo njiani.

Muscab alieleza kuwa Kenya ndio adui yao mkubwa katika ukanda huu na kuonya kuwa shambulizi la Westgate si lolote mbele ya yatakayotokea iwapo Kenya haitaondoka Somalia.


“Kenya ni adui yetu wa kihistoria. Kenya ni adui wa watu wa Somalia na nchi ya Somalia. Hatuamini kama Kenya ni jirani mwema. Hatuwaamini na tutawapiga sana kwa sababu ni adui zetu”, alisema Muscab.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.