BOMU LAUA MAKUMI YA WATU NJE YA KANISA NCHINI PAKISTAN


The site of a bomb attack in Peshawar, Pakistan (file photo)


WATU sabini wamepotez maisha katika mlipuko wa bomu uliotokea nje ya kanisa moja katika mji wa kaskazini magharibi wa Peshawar nchini Pakistan.

Maafisa wanasema kuwa shambulio hilo lilitokea katika Wilaya ya Koshati Gati. Mabomu mawili yalilipuka wakati waamini wakitoka kwenye ibada katika Kanisa hilo Kongwe nchini humo.

Maafisa hao wansema kuwa watu wapatao 100 wakiwemo wanawake na watoto walijeruhiwa katika shambulizi hilo.

Hakuna kundi lililodai kuhusika, ingawa baadhi ya makundi ya wapiganaji yamekuwa yakilaumiwa kwa mashambulizi yaliyotokea huko nyuma dhidi ya Wakristo wachache katika taifa hilo.

Maelfu ya Wapakistan wamepoteza maisha yao katika milipuko ya mabomu na mashambulizi mengine yanayofanywa na wanamgambo tokea mwaka 2001, baada ya nchi hiyo kuunda ushirika na mataifa ya kigeni katika vita dhidi ya ugaidi.

Maelfu ya watu wamepoteza makazi kutokana na wimbi la ghasia na uasi unaotikisa maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.