KENYATTA AANZISHA MGOGORO NA UMOJA WA MATAIFA
KWA mara ya kwanza tangu kujipatia uhuru wake, Kenya haitawakilishwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya Nairobi, Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja huo, Machariah Kamau, alimtaarifu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon kuwa Kenya haitahudhuria kwenye Hadhara Kuu inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Rais Kenyatta asingeweza kuwa nje ya nchi wakati ambao Makamu wake pia hayupo nchini. Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto yuko nchini Uholanzi akihudhuria vikao vya kesi inayomkabili kwenye mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Wiki moja kabla ya kuanza kwa kesi ya Ruto, Kenyatta alikuwa ameonesha kuwa isingewezekana kwa viongozi wote wawili kuwa kuwa nje ya nchi kwa wakati mmoja. Wakati huo ICC ilikuwa imeshatoa ratiba ya awali iliyoonesha kuwa wote wawili wangeweza kuwa mahakamani kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kenya ilimwambia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa nafasi ya kisiasa ya kuendelea uhusiano ilikuwa ikizorota na nchi hiyo ilikuwa ikihofia matokeo mabaya kutokana na mwenendo wa waendesha mashitaka wa ICC.

Kenyatta alikuwa amepangiwa kuhudhuria Kikao cha Mkutano Mkuu wa Umaoja wa Mataifa kuanzia Septemba 23 mpaka Septemba 27.Aidha, Rais Kenyatta amemwita Nairobi Balozi wa Kenya kwenye Umoja huo, Macharia Kamau, kwa mashauriano. 
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.