MAHOJIANO YA MSEMAJI WA AL-SHABAAB KUHUSU UVAMIZI ULIOTOKEA KENYA

 

MWANDISHI Jaman Osman alifanya mahojiano maalumu na msemaji wa kundi la Al-Shabaab kuhusiana na sababu za kukishambulia kituo cha biashara cha Westgate, mjini Nairobi.


Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano hayo yaliyofanywa kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Channel4

JAMAL OSMAN: Kwa nini mlifanya shambulio?


MSEMAJI: Sababu ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu, kwa sababu Kenya ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu. Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na tunajilinda.

Haidhuru kama wewe ni Muislamu au Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule anayekushambulia.

JO: Mumeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?


MSEMAJI: Tumewaambia Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile ambacho Kenya inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda na tuliwaonya kuhusu kwenda Kenya.

Wakenya wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya lazima ajiandae kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa Ulaya ama wa Marekani, kwa sababu sisi si dhaifu.

Na tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao kama mnataka kuwa salama.


JO: Kwa nini mliliilenga Westgate?


MSEMAJI: Sababu ya kuielenga Westgate ni kwa kuwa Wakenya na serikali yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu, popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo.

Sababu ya kuilenga Westgate ni kwamba, tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia maumivu zaidi. Ni kwa sababu inaingiza pesa nyingi na ipo katikati ya jiji.

Ni sehemu inayowaumiza zaidi na kwa sababu tulitaka kutuma ujumbe na hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikie kila Mkenya.

JO: Wapiganaji wenu ndani ya Jengo bado wanapigana?


MSEMAJI: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.


JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?


MSEMAJI: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.


JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini yatakuwa matokeo ya hili?


MSEMAJI: Kama Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata ujumbe kwamba kama ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa hawawezi kuishikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategee waishi kwa amani Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kutuma kwao.


JO: Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mumeshifikia malengo yenu?


MSEMAJI: Tunaiambia Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.


JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya ni kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?


MSEMAJI: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuaiacha nchi yetu.


JO: Kwa nini mnalenga watu wasio na hatia?


MSEMAJI: Raia wa kigeni wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo (Kenya) kwa sababu Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila mtu- Kenya ni eneo la vita.


JO: Kwa kuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?


MSEMAJI: Tunawaambia Waingereza, kwa kuwa tunaamini wanawasaidia Wakenya na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya walitoe jeshi lao Somalia.


Na Waingereza wanajua Wasomali hawatakata tamaa. Tuliwakatalia Waingereza huko nyuma, ambao wana nguvu kuliko Wakenya. 


(Kwa hisani ya mashirika ya habari)
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.