MAMA AMNG’ATA BINTIYE SEHEMU ZA SIRI


MKAZI wa Kijiji cha Mlongazila, wilayani Kisarawe, Pwani, Moshi Hamad anatuhumiwa kumng’ata mwanaye, Khadija Hamad (6) sehemu za siri kwa madai ya kujisaidia haja kubwa na ndogo hovyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima juzi wilayani Kisarawe, wakazi hao walisema mama huyo amekuwa na tabia ya kumfungia ndani mtoto wake huyo na kumchapa kwa zaidi ya nusu saa, akitumia nyaya za simu na kumng’ata sehemu mbalimbali za mwili zikiwamo za siri na kumsababishia maumivu makali.

Wakazi hao walisema waliamua kutoa taarifa kwenye dawati la haki za binadamu baada ya kuchoshwa na vitendo hivyo, na sasa wamelitaka Jeshi la Polisi kumkamata mama huyo na kumchukulia hatua.

Stella Musa, alisema sehemu za siri za mtoto huyo zimeharibiwa kutokana na kung’atwa na meno, huku zikiwa na vidonda vinavyodaiwa vimetokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali.

“Wazazi wa mtoto huyo ni wanangu, siku moja mama huyo alimuumiza mkono. Nilimchukua na kukaa naye nyumbani kwangu kwa mwezi mmoja nikimuhudumia kwa kumkanda kwa maji ya moto,” alisema Stella.

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mlongazila, Paulo Idana ambaye pia ni katibu wa dawati la kutetea haki za binadamu, alisema suala hilo limewafikia, hivyo wanachukua hatua za kisheria huku mtoto huyo amewekwa chini yao kwa matibabu zaidi.

“Tulimfuata mama huyo Septemba 20 mwaka huu na tulifanya nae mahojiano mbele ya ofisa mtendaji wa kijiji na alikiri akisema alifanya hivyo kwa sababu ya hasira. Tunafanya utaratibu ili tumfikishe kwenye vyombo vya sheria,” alisema Idana.

Akieleza mkasa huo, mtoto huyo alisema wakati mwingine mama yake alikuwa akimwita ili amfundishe kusoma na aliposhindwa aling’atwa mgongoni, mapajani na sehemu za siri huku akisema atamfanyia hivyo hadi ajue kusoma.

Mama wa mtoto huyo, Moshi, alisema alikuwa akitoa adhabu kwa mwanaye huyo kutokana na kujisaidia haja ndogo na kubwa hovyo wakati akirudi shule.

“Nafanya hivi kutokana na hasira siwezi nikamuona mtoto wangu anajisaidia haja kubwa na ndogo kwenye nguo nikamwacha tu, lazima nimwadhibu… jana alitapika kwenye sahani. Je, mtoto kama huyu nitamwacha?” alihoji Moshi.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Khadija Samizi alikiri kuwepo kwa tukio hilo.Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.