NAIBU WAZIRI WA ELIMU AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMBAKA MWANAFUNZI

 Naibu Waziri wa Elimu nchini Sierra Leone, Mamoud Tarawali ameshitakiwa kwa makosa ya kumbaka mwanafunzi wa chuo kikuu, polisi walisema.

"Anakabiliwa na mashitaka ya kubaka, kujeruhi, kushambulia na kudhuru kwa kukusudia. Amenyimwa dhamana na sasa yupo katika jela ya Pademba,” mkuu wa polisi Francis Munu, alisema siku ya Jumanne.

Wiki iliyopita, Tarawali alifikishwa kwa pilato kwa tuhuma za ubakaji. Siku ya Jumatatu alikuwa mahakamani kusikiliza mashitaka yakisomwa na aliyanusha yote.

Polisi wanasema kuwa mashitaka hayo yaliwasilishwa na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 24 kutoka chuo kikuu cha Sierra Leone cha mjini Freetown aliyesema kuwa alibakwa na Tarawali katika eneo la faragha.

Sierra Leone inajaribu kuponya majeraha ya vita vya muda mrefu, ambapo wapiganaji walifanya kila aina ya dhulma za kingono dhidi ya wanawake na mabinti na matukio hayo yakashamiri.


- Reuters
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.