OBAMA AZUNGUMZA NA RAIS WA IRAN

Iranian President Hassan Rouhani (R) and his American counterpart Barack Obama
Rais wa Iran, Hassan Rouhani (kulia) na Rais Barack Obama wa Marekani (kushoto)RAIS wa Iran  bwana Hassan Rouhani na mwenzake wa Marekani bwana Barack Obama wamefanya mazungumzo kwa njia ya simu wakati rais wa Iran akikamilisha ziara yake kwenye hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.

Shirika la habari la Iran, IRNA, limeripota kuwa Rouhani alipokea simu kutoka kwa Rais Obama leo Ijumaa wakati akielekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa John F. Kennedy kwa safari ya kurejea Tehran.

Viongozi hao walisisitiza juu ya utashi wa kisiasa wa nchi zao kutafuta muafaka  juu ya programu ya nyuklia ya Iran, na walibadilishana mawazo kuhusu mambo kadhaa, ikiwemo ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kieneo.

Aidha, wakati wa mazungumzo hao, waliwapa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa nchi hizo, bwana Mohammad Javad Zarif wa Iran na bwana John Kerry wa Marekani, jukumu la kuandaa uwanja kwa ajili ya ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.

Mazungumzo hayo ya simu ni ya kwanza baina ya marais wa nchi hizo mbili tangu mapinduzi ya Iran ya mwaka 1979, na yamefanyika kufuatia kikao cha jana Alhamisi baina ya Iran na mataifa sita yenye nguvu uliofanyika mjini New York kuhusu programu ya nyuklia ya Iran.

Kerry aliyaita mazungumzo hayo kuwa “yenye kujenga,” akisema, “tumekubaliana kufanya juhudi ya kuendelea na mchakato utakaotengeneza msingi na kutafuta njia ya kupata majibu ya maswali ambayo watu wanayo kuhusu programu ya Nyuklia ya Iran.”

Naye waziri wa mashauri ya kigeni wa Iran, Muhammad Zarif, aliyasifu mazungumzo hayo kama “mazuri sana na yenye mafanikio” na kusema kuwa matokeo ya mazungumzo hayo yalijumuisha suala la “kuondosha kabisa” vikwazo vyote dhidi ya Iran.

“Tunatumai tutaweza kupiga hatua kulitafutia ufumbuzi suala hili na kuhakikisha kuwa hakuna wasiwasi juu ya program ya Iran ambayo ni ya amani,” alisema bwana Zarif.

Iran imekuwa ikituhumiwa na mataifa ya Magharibi na wataifaki wao kuwa programu yake ya nishati ya nyuklia inalenga kutengeneza silaha za maangamizi.

Hata hivyo, Iran imekuwa ikikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa mradi wake huo ni kwa ajili ya malengo ya amani.


CHANZO: Press Tv
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.