SAMANTHA LEWTHWAITE ALIWAHI KUJA TANZANIA
Mwanamke anayedaiwa kuongoza kundi la wavamizi lililovamia jengo la kibiashara la Westgate, Samantha Lewthwaite inadhaniwa kuwa ameuawa.

Lewthwaite, ambaye anaitwa kwa jina la utani la ‘Mjane Mweupe’ anadaiwa kuongoza shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu 62 na kujeruhi wengine 170 mjini Nairobi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, mwanamke huyo inasemekana aliuawa juzi usiku na wanajeshi wa Kenya wanaoshirikiana na maofisa wa Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) na wale wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).

Hata hivyo, viongozi wa usalama wa Kenya hawakutaka kuingia kwa undani juu ya taarifa za kifo cha Lewthwaite.

Kwa muda mrefu, Lewthwaite amekuwa akiwakimbia polisi kwa kuvaa hijab akitembelea kati ya nchi za Tanzania, Somalia na Kenya.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, mwanamke huyo amekuwa akiishi kwa kujificha na amefanikiwa kutumia pasi za kusafiria za nchi tofauti.


Amekuwa akitambulika kama raia wa Uingereza na Australia lakini inasemekana amekuwa pia akitumia pasi ya kusafiria inayoonyesha kwamba yeye ni raia wa Afrika Kusini akitumia jina bandia la Natalie Faye.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.