SAMANTHA LEWTHWAITE: ‘MJANE MWEUPE’ MWENYE ASILIA YA UINGEREZA ANAYEDAIWA KUPANGA SHAMBULIZI LA KENYA

 


Samantha Lewthwaite, mwanamke mwenye asili ya Uingereza, anayejulikana katika  vyombo vya habari ya Uingereza kama “Mjane Mweupe,” ameibuka kuwa mshukiwa mkuu katika shambulizi la hivi karibuni katika Jumba la Kibiashara la Westgate, jijini Nairobi nchini Kenya.

Mwanamke huyo mtoto wa askari wa Uingereza, Lewthwaite, makuzi yake yalikuwa ya “kawaida” na akiwa na umri wa miaka 17 alikutana na Germaine, ambaye alikuwa raia wa Uingereza mwenye asili ya Jamaica. Wawili hao walikutana kwenye mtandao wa intaneti na baada ya miaka 3 wakaoana.

Lindsay alikuwa mmoja wa watu wanne wanaodaiwa kuhusika na milipuko ya mwaka 2005 nchini Uingereza iliyoua watu 52. Wakati huo, Lewthwaite alilaani shambulizi hilo lililofanywa na marehemu mumewe, akisema kuwa akili ya mumewe huyo ilikuwa imethiriwa na sumu ya watu wenye misimamo mikali.

MOYO WAKE ULIVYOBADILIKA

Katika mabadiliko yanayoonekana kutokea katika moyo wake, anashukiwa kuwa amehusika katika mashambulizi mbalimbali katika eneo la Afrika Mashariki, ambapo matata yake mapya yameonekana katika kuratibu shambuli la  wanamgambo wa al-Shabaab katika mauaji ya watu zaidi ya 60 katika kituo cha biashara mjini Nairobi.

Taarifa zinasema kuwa, mwaka 2007, Lewthwaite alielekea Kenya pamoja na watoto wake watatu, akakata mawasiliano yake yote na familia yake na kujiingiza katika mitandao inayodaiwa kuwa ya kigaidi.

Duru za kiusalama zinadokeza kuwa Lewthwaite ni “mshukiwa namba moja” katika msako unaofanywa na polisi ya Kenya.

Afisa mmoja katika kitengo cha kupambana na ugaidi anasema kuwa walimshuku  Lewthwaite kuwa ndiye aliyeratibu shambulizi hilo baada ya manusura kueleza kuwa walimuona mwanamke aliyejifunika usoni akitoa amri kwa wapiganaji wa  al-Shabaab wakati walipowashambulia watu katika Jumba la Westgate.

Vilevile, Lewthwaite anatuhumiwa kuwa huko nyuma aliwahi kuwapa mafunzo wanawake wanaojilipua nchini Somalia na kufanya kazia kama mzungumzaji rasmi wa al-Shabaab.

‘MWANAMKE MWEUPE’

Msemaji wa serikali ya Kenya alisema kuwa manusura wa tukio hilo walimuona “mwanamke mweupe” akiwa miongoni mwa watekaji. Msemaji huyo alipoulizwa kama huyo “mwanamke mweupe” ni Lewthwaite, akasema kuwa “inawezekana lakini haijathibitishwa”.

Katika ujumbe kwenye ukurasa wa Twitter,  al-Shabaab walimsifu Mjane Mweupe na kufurahia kuwa Lewthwaite alikuwa pamoja nao.


Ujumbe huu: “sherafiyah lewthwaite aka samantha is a vrave [sic] lady! were happier to have her in our ranks!” waliuweka kwenye akaunti yao rasmi ya @HSM_Press kabla ya kuufuta.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.