WATU 15 WAKIWEMO WATOTO 13 WAMEKUFA MAJI KATIKA ZIWA TANGANYIKA

 

Watu 15 wakiwemo watoto 13 wamekufa maji katika Ziwa Tanganyika, baada ya mtumbwi mkubwa waliokuwa wakisafiria kutoka kwenye kijiji cha Kipwa katika wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa , kuelekea katika kijiji cha Kapele  kufuata huduma za kliniki kupinduka ndani ya ziwa hilo.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Kalambo Dakta Hosea Mang'ombe, amesema kufuatia kijiji cha Kipwa kilichoko kwenye mwambao wa ziwa Tanganyika kukosa huduma ya zahanati, wananchi wa kijiji hicho wamejiwekea utaratibu wa kupata huduma hiyo kwenye kijiji cha Kapele kilichoko umbali wa zaidi ya kilonita 10, na ndipo walipokumbwa na balaa hilo ambapo pia wanahisi kuwepo kwa mama mjamzito ambaye hadi sasa hajaonekana .


akithibitisha kuhusu tukio hilo kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda, amesema jeshi hilo linaendelea kuchunguza juu ya ajali hiyo mbaya, na kutafuta miili ya baadhi ya watu ambao walikuwa hawajapatikana bado hadi sasa.


CHANZO: ITV
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.