WAZIRI MKUU WA SOMALIA: TOTAWAANGAMIZA AL-SHABAAB


Somali Prime Minister Abdi Farah Shirdon SaaidWAZIRI Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon ameapa “kuwafuta” al-Shabaab waliotekeleza shambulizi kwenye jengo moja la kibiashara nchini Kenya.

"Tuna zaidi ya askari 17,000 wa AMISOM (askari wa Umoja wa Afrika) nchini Somalia na kwa kusaidiana na wananchi wetu na jumuiya ya kimataifa, nina imani tutawamaliza al-Shabab," anasema bwana Shirdon.

Anasema kuwa nchi yake kwa kushirikiana na Kenya wataendelea kupambana na wapiganaji hao kwa kuwa ni tatizo linalozisibu nchi hizo kwa pamoja na kwamba Mogadishu haitakubaliana na matakwa ya al-Shabaab ya kutaka vikosi vya Kenya viondoke Somalia:
 “Tatizo la Al-Shabab sio tatizo la Somalia peke yake, ni tatizo ya ukanda mzima, na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla…tunapambana na adui yetu sote.


"Hatuna tatizo na ndugu zetu wa Kenya…Wapo Somalia kwa ombi la Somalia, wapo kama sehemu ya jeshi la AMISOM na tunashirikiana katika kupambana na al-Shabaab,” alisema.

Aliongeza kusema kuwa, “Nina furaha kwamba tutawadhibiti na hivi karibuni hawatatusumbua tena, inshaallah.”

Mapema Jumamosi, wapiganaji wa al-Shabab walifanya shambulio kwenye jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi, ambalo hatimaye lilikombolewa mapema Jumanne.

Kwa uchache raia 61 na wanajeshi 6 waliuawa katika shambulizi hilo. Idadi ya mwisho ya vifo bado haijatangazwa.


Kundi la al-Shabab lilidai kuhusika na shambulio hilo, likisema kuwa walifanya hivyo kujibu mapigo ya uwepo wa askari wa Kenya nchini Somalia.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.