BOMU LALIPUKA KATIKA KAMBI YA JESHI

Smoke billows following a car bomb blast targeting a Libyan army camp in Benghazi on April 29, 2014.
Moshi mkubwa ukifuka baada ya bomu lililolipuka kwenye kambi ya jeshi la Libya mjini Benghazi leo Aprili 29, 2014. 

Mlipuko wa bomu la kutegwa kwenye gari katika kambi ya jeshi kwenye mji wa Benghazi nchini Libya umeua askari wawili.

Maafisa nchini humo wanasema kuwa mlipuko huo umetokea kwenye lango la kambi ya vikosi maalumu jirani na uwanja wa ndege wa mji huo.

Hata hivyo, hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Mji wa Benghazi umekuwa ukishuhudia matukio mengi ya mashambulizi na mauaji ya kisiasa kutokana na makundi ya waasi waliomng’oa Kanali Muammar Gaddafi kuingia katika vita vya kugombania madaraka.

Mnamo Machi 17, askari kumi waliuawa katika mfululizo wa milipuko ya mabomu ya kutegwa kwenye magari ambayo iliitikisa kambi moja ya jeshi katika mji huo.

Mwezi mmoja baadaye, watoto kumi na mbili walijeruhiwa katika mlipuko ndani ya ndani ya shule moja mjini Benghazi baada ya mtu mmoja aliyekuwa kwenye hari kurusha bomu katika shule hiyo.


Miaka mitatu baada ya kuanguka kwa Kanali Gaddafi, nchi hiyo bado imeendeea kukumbwa na hali ya ukosefu wa usalama baada ya waasi waliomuondoa Gaddafi kukataa kuweka silaha chini licha ya juhudi za serikali kuu kujaribu kuweka sheria na kudhibiti hali ya mambo.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.