NAPE NA KINANA KUMBE NI MAFUNDI UJENZI? WASHUHUDIE WAKIWAJENGEA GHALA LA KUHIFADHIA MAZAO YA CHAKULA WANACHI WA KIGOMA VIJIJINI.

Katibu Mkuu wa CCM Bw. Abdulkarim Kinana na Katibu wa NEC ~CCM wa Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye kwa pamoja wakishiriki ujenzi wa Ghala la kuhifadhia chakula na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha Kidahwe kilichopo Wilaya ya  Kigoma Vijijini~ mkoa wa Kigoma.
 (kama wanavyo onekana pichanihapo juu).  
Gharama za mradi huo ni shilingi 104, 800,000, Ghala hilo linalenga kuhifadhia mazao ya wakulima wa kijiji hicho baada ya kuvuna yao ili kusubiri soko na bei nzuri ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ya Ghalani.
Usimikaji wa Mashine katika Ghala hilo pia utawasaidia Wanakijiji kuweza kusaga mazao kama Mahindi, Muhogo na nafaka zingine kwa kupata unga na kuuza.


Katibu Mkuu wa CCM Bw. Kinana akishirikiana na wananchi kufukia mabomba ya mradi wa maji katika Kijiji cha Nkungwe wilaya yaKigoma Vijijini mkoani Kigoma. Juu pichani ni tank hilo linaloendela kujengwa kama linavyoonekana ujenzi wakebado unaendelea, mradi huo wamaji utakapokamilika uanatarajia kuvisaidia Vijiji zaidi ya 30.
Katibu Mkuu wa CCM akiwasomea wanchi wa Mahembe orodha ya Vijiji vitakavyopatiwa maji na umeme katika wilaya ya Kigoma vijijini.
Katibu wa NEC~ CCM wa Itikadi na Uenezi Bw. Nape Nnauye katikati akawahutbiwa wananchi wa kata ya Mahembe katika jimbo la Kigoma Kaskazini.
Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.