RAIS DKT.JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA KIFO CHA ALIEKUWA WAZIRI MKUU WA ZAMANI HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE.

     Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo ameliongoza taifa katika maadhimisho ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa  Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine katika maadhimisho yaliyofanyika nyumbani kwake  Monduli Juu.  Pichani ni juu ni Rais Dkt. JakayaMrisho  Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa kumbukumbu ya miaka 30 tangu kifo chake.


               Rais Mstaafu, Benjamini Mkapa akiweka shada la maua  katika kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania                                                             Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa kumbukumbu ya miaka 30 tangu kifo chake.
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa akiweka shada la maua katika Kaburi la                      aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania   Hayati  Edward Moringe Sokoine .

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na wajane wa alieyekuwa Waziri Mkuu wa Zamani Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa kumbukumbu ya Kiongozi huyo wa zamani wa Tanzania. Wengine kutoka kushoto ni Mjane wa baba wa Taifa, mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Spika wa Bunge, Anne Makinda namototo wa Hayati Sokoine Ndugu Joseph Sokoine.
                                                          (Picha tumezipata kupitia Dotto Mwaibale blog).
Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.