SHAMBULIZI LA BOMU LAUA 4 MJINI NAIROBI
Kwa uchache watu wanne wakiwemo maafisa wawili wa polisi wameuawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Polisi wamesema kuwa mlipuko huo umetokea nje ya kituo cha polisi Pangani mjini humo.

Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi hiyo, imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bomu hilo lilitegwa katika gari aina ya saloon.

Mpaka sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo. Lakini polisi wanasema kuwa mitaa hiyo iliwahi kushuhudia mashambulizi kama hayo.

Katika miezi ya hivi karibuni Kenya imekumbwa na mashambulizi kadhaa ya mabomu.


Mwezi Septemba mwaka jana, shambulizi kwenye jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi liliwaua watu wasiopungua 67.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.