MOTO WATEKETEZA NYUMBA IRINGA , MAMA MWENYE NYUMBA APOTEZA FAHAMU.

           Wasamaria wema  wakazi wa Zizi la Ng'ombe mjini              Iringa  wakimsaidia  kumnywesha  dawa Bi Grace Mpewa baada ya kupoteza fahamu  kutokana  na moto  kuteketeza  nyumba  yake leo mchana tare 25.04.2014.

                                            Baadhi ta mali zilizo teketea kwa moto huo.

Baadhi ya wananchi wakiangalia mali zilizo ungua ndani ya nyuba.
Gari  la  kikosi  cha  zimamoto na uokoaji Manispaa ya  Iringa likizima moto  uliokuwa ukiteketeza  nyumba ya mkazi wa Zizi la Ng'ombe Bi Grace Mpewa  leo majira ya mchana chanzo cha moto huo ni mtoto kuchezea moto mali mbali mbali ziliteketea  katika  tukio hilo.
Pichani chini ni askari wa zima moto wakiaangalia baadhi ya mali zilizo ungua katika nyumba hiyo.

MOTO  mkubwa  umezuka  katika  nyumba  ya mkazi  mmoja  wa  eneo la Zizi la Ng'ombe katika Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa na kupelekea mtu mmoja kupoteza  fahamu  baada ya  nyumba yake  kuwaka  moto mchana  wa leo tarehe 25.04 .2014.
Mashuhuda wa  tukio   hilo  wameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.com  kuwa  moto  huo  chanzo chake  kimesababishwa na mtoto mdogo  ambae  alikuwa  ndani ya  nyumba  hiyo akichezea  moto ndani ya  nyumba  hiyo na  kusababisha  moto  huo kushika makochi yaliyokuwemo ndani ya  nyumba  hiyo.

Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.