AJALI YA KIVUKO YAUA MAMIA YA WATU

 


Miili ya watu 12 imeopolewa baada ya kivuko kilichokuwa na abiria kupinduka na kuzama nchini Bangladesh ya kupigwa na dhoruba kali.

Maafisa wanasema kuwa kivuko hicho kilikuwa kimeondoka katika kituo kikuu cha Dhaka na kilizama saa kadhaa baada ya kuanza safari yake.

Baadhi ya abiria waliogelea mpaka nchi kavu huku wengine wakiwa hawajulikani waliko. Wengine kadhaa waliokuwa wakielea katika mto Meghna waliokolewa na waokoaji.
Polisi wanasema wanawake na watoto ni miongoni mwa waliokufa.

Idadi ya vifo inaweza kupngezeka kwa kuwa kazi ya uokoaji inaendelea na kuna uwezekano wa kuopoa miili mingi zaidi.


Matukio ya ajali za vivuko yamekuwa yakiikumba Bangladesh kwa sababu ya msongamano wa abiria na mfumo mbovu wa usimamizi wa huduma hiyo.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.