AJARIBU KUINGIA IKULU AKIWA UCHIMtu huyo alisisitiza kuwa alikuwa na miadi ya kukutana na Rais Obama

Wanausalama wa Ikulu ya Marekani wamemkamata mtu mmoja aliyevua nguo na kutaka kuingia kuparamia uzio wa Ikulu hiyo.

Mtu huyo alikamatwa nje ya makazi rasmi ya rais wa Marekani jana Ijumaa na picha zinawaonesha wanausalama wasiopungua wanne wakimdhibiti mtu huyo nje ya jengo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Caller, mtu huyo alijaribu kusogea kwenye geti la walinzi wa Ikulu na kusisitiza kuwa alikuwa na miadi ya kuonana na Rais Obama.

Alipokataliwa kuingia alianza kuvua nguo zake mbele ya geti huku akisema, “nina miadi ya kukutana na Rais Obama saa tisa alasiri!”


Wanausalama walimkamata, magari ya zimamoto na yale ya polisi akafika mara moja na kizuizi kikawekwa nje ya Ikulu na mtaa Pennsylvania Avenue ukafungwa.

Mapema mwezi huu, watu wawili walikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya “kutupa vitu” kwenye uzio wa Ikulu muda kama huo huo.


Mtu mmoja alitupa kitu kilichosadikiwa kuwa ni mkanda wa kaseti kwenye uzio huo upande wa kaskazini huku mwingine akidaiwa kutupa karatasi katika eneo la upande wa kusini.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.