AL-SHABAAB: TUNAHAMISHIA VITA KENYA

Polisi wa Kenya wakiwa katika eneo la Gikomba mjini Nairobi ambapo milipuko pacha iligharimu maisha ya watu kumi na wengine zaidi ya sabini kujeruhiwa Ijumaa iliyopita.Kundi la wapiganaji wa Al-Shabaab la nchini Somalia limeapa kuhamishia mpambano yake katika nchi jirani ya Kenya.

Mmoja wa makamanda waandamizi wa kundi hilo, Fuad Mohamed Khalaf, alisema wakati akiwahamasisha wapiganaji wake katika matangazo ya radio:
“Vita vitahamia Kenya, wakiua binti wa Kisomali nasi tutaua binti wa Kenya.”

“Tunawataka Waislamu wote nchini Kenya… kupambana na serikali ya Kenya ndani ya nchi hiyo, kwa sababu Wakenya waliua watu wetu wakiwemo watoto,” alisema Khalaf katika matangazo ya Radio Andalus inayomilikiwa na Al-Shabaab.

Askari wa Kenya waliingia kusini mwa Somalia mwaka 2011 kuwakabili wapiganaji wa Al-Shabaab na kisha wakaungana na kikosi cha Umoja wa Afrika kinachopambana na wapiganaji hao.

Wiki hii ndege za kivita, zinazosadikiwa kutoka Kenya, zilishambulia ngome za Al-Shabaab, kama sehemu ya harakati ya kikosi cha Umoja wa Afrika dhidi ya waasi hao.

“Askari wao na ndege zao zikiua watu wenu, Mungu amewaruhusu kulipiza sawia, tutapambana na Wakenya,” alisema Khalaf, ambaye anatazamwa kama mtu wa pili kwa umuhimu baada ya kiongozi wa al-Shabaab, Ahmed Abdi Godane.

Wapiganaji wa Al-Shabaab, ambao walidai kuhusika na shambulizi la mwezi Septemba 2003 kwenye jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu wasiopungua 67, wamekuwa wakilaumiwa kwa milipuko na mashambulizi kadhaa ya mabomu ambayo yamekuwa yakiua watu nchini humo.

Wiki iliyopita, shambulizi la bomu kwenye soko moja mjini Nairobi liliwaua watu 10 na kujeruhi wengine kadhaa, huku Marekani ikisema kuwa inaandaa kupunguza wafanyakazi wake nchini Kenya kwa sababu ya ongezeko la vitisho vya mshambulizi.

Al-Shabaab walisema kuwa wapiganaji wake ndio waliofanya shambulizi baya la kushtukiza la siku ya Jumatatu dhidi ya msafara wa jeshi la Kenya katika mji wa kaskazini mashariki wa Mandera, jirani na mpaka wa nchi hiyo na Somalia.

Khalaf alisema kuwa Al-Shabaab imewaandaa wapiganaji wengi na kuapa kuwa watatumwa kufanya mashambulizi ndani ya Kenya.


“Tumewapa mafunzo watu wetu…. Ndio waliofanya shambulizi la Mandera,” alisema na kuongeza: “Wengi zaidi watatumwa hivi karibuni.”
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.