ALIYEJARIBU KUMUUA OBAMA AFUNGWA MIAKA 25

US President Barack Obama
Rais wa Marekani Barack ObamaMtu mmoja kutoka Mississippi aliyekiri kosa la kutuma barua zenye sumu kwa Rais Barack Obama na maofisa wengine amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela.

James Everett Dutschke alikiri kutenda kosa hilo mwezi Januari kwamba aliwatumia barua zenye sumu kali Rais Obama, Seneta wa Mississippi Roger Wicker na Jaji  Sadie Holland. Baadaye aliikana kauli yake, lakini wiki iliyopita aliirejea tena ili kukwepa adhabu ya kifo kama angekutwa na hatia.


Aidha, Dutschke atatumikia adhabu ya kifungo cha nje cha miaka 5 akiwa chini ya uangalizi maalumu atakapotoka gerezani. Wakati huo atakuwa na umri wa miaka 66.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.