BALOZI WA MALAWI NCHINI TANZANIA AFARIKI LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Balozi wa Malawi nchi Tanzania Mhe. Flossy Gomile Chidyaonga pichani afariki dunia leo tarehe 09.04.2014 jijini Dar es Salaam baada ya kuuguwa kwa muda mfupi.

"Kwa masikitiko makubwa sana Wizara ya nchi za nje na Ushirikiano wa Kimatafa ya Malawi inauarifu   Umma kufariki dunia kwa Balozi wake nchini  Tanzania Mhe. Flossy Gomile Chidyaonga, baada ya kuuguwa kwa muda mfupi jijini Dar es Salaam mchana wa tarehe 09.04.2014", imesema taarifa  iliyotolewa na msemaji wa Wizara hiyo Quent Kalichero.

'Tangu mwaka 2006 Marehem  Flossy Gomile alikuwa Naibu Balozi  wa Malawi London kabla ya kuteuliwa kuwa balozi wa Malawi nchini Tanzania mwezi september mwaka 2011". Imesema taarifa hiyo na kuongeza kuwa taratibu za mazishi zitatangazwa baada ta taratibu kukamilika.
Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.