BAN KI-MOON AWASILI SUDAN KUSINI


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewasili leo Sudan Kusini. Kiongozi huyo anatarajiwa kukutana na Rais Salva Kiir, watu walioyakimbia makazi, viongozi wa kijamii na wafanyakazi na walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Aidha, anatarajiwa kutoa wito wa kukomeshwa mapigano ambayo yamepoteza maisha ya watu wengi ambapo viongozi wamepuuza juhudi za kuleta amani licha ya onyo na tahadhari ambazo zimekuwa zikitolewa kuhusu mauaji ya kimbari na ukosefu wa chakula.


Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.