BUNGE LA SOMALIA LASHAMBULIWA
Kwa uchache watu kumi wamepoteza maisha baada ya shambulizi lililofanywa kwenye jengo la bunge la Somalia mjini Mogadishu.

Kwa mujibu wa polisi nchini humo, washambuliaji walilipua mabomu mawili wakati wakijaribu kuingia katika eneo la bunge leo hii.

Silaha nzito zilisikika kufuatia milipuko hiyo, wakati wabunge wakiwa ndani ya jengo.

Kwa uchache walinzi wanne na waasi sita wameuawa na wengine kadhaa, wakiwemo wabunge wawili, wamejruhiwa.

Kundi la Al-Shabab limedai kuhusika na shambulizi hilo ambalo limewafanya baadhi ya wabunge kulilaumu jeshi la nchi hiyo kuwa limeshindwa kuwalinda.

Kundi hilo limeshafanya mashambulizi kama hayo mjini Mogadishu, ikiwemo mahakama kuu na ikulu ya rais.

Kwa miezi kadhaa Somalia imekuwa ikikumbwa na ghasia mbaya, ikiwa ni pamoja na mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa mashirika ya misaada.

Mnamo Juni 2013, wapiganaji wa kundi hilo walizishambulia ofisi za Umoja wa Mataifa katikati ya mji wa Mogadishu. Shambulizi hilo liligharimu maisha ya watu wasiopungua 15.

Kikosi cha Umoja wa Afrika (AMISOM) kinachoundwa na askari kutoka Uganda, Burundi, Djibouti, Sierra Leone na Kenya kiliwaondosha wapiganaji wa Al-Shabab kutoka mjini Mogadishu na miji mingine mikubwa nchini humo.


Somalia haikuwa na serikali kuu yenye ngumu tangu mwaka 1991 mpaka Agosti 2012. Mwezi Septemba 2012, wabunge wa Somalia walimchagua Hassan Sheikh Mohamud kuwa rais mpya wa nchi hiyo.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.