JIFUNZE JINSI YA KUANDAA SALADI YA TAMBI NA JIBINI (cheese)Kuna tambi za aina mbalimbali, zenye ladha na maumbo tofauti. Upishi wake nao  unatofautiana kutokana na aina ya tambi. Unaweza kuandaa tambi kama chakula kikuu, kama salad, au kama kitafunwa, kutokana tu na aina ya tambi utakayochagua na jinsi utakavyoiandaa.

MAHITAJI
  • Tambi paketi 1 -zenye umbo la spring
  • Jibini kavu kikombe 1: Sugua kwa sugulio la karoti (shred)
  • pilipili hoho za kijani 3 kubwa- kata vipande vinene kwa urefu
  • Pilipili hoho nyekundu Moj: kata vipande vinene kwa urefu kisha gawanya kila kipande mara mbili
  • Giligiliani kavu kijiko 1 cha chakula : saga mbegu kavu za giligiliani

NJIA

1.    Chemsha maji  mengi hadi yatokote (lita mbili). Ongeza tambi, acha zichemke hadi ziive .
  • Usiache ziwe rojo hazitapendeza
2.    Katika kikaango au sufuria zito weka pilipili hoho za rangi zote, kisha weka jikoni katika moto mdogo, geuza kila mara hadi zote zipate joto na kuanza kusinyaa kisha weka pembeni
  •   Usiongeze kitu chochote kwenye pilipili hoho
3.    Tambi zikiiva chuja maji yote kisha weka tambi kwenye bakuli la chuma au sufuria pana
  •     Chuja maji mara tu tambi zikiiva, usiache zipoe wala kupoteza joto
4.    Katika bakuli la tambi ongeza pilipili hoho. Nyunyuzia chumvi na unga wa giligiliani kisha nyunyuzia jibini na changanya vizuri.
Saladi yako iko tayari kwa kula. Unaweza kula salad hii na vyakula vingine au ukaifanya sehem kuu ya mlo wako. Ni vyema kujua kwamba saladi si lazima ziwe mboga za majani peke yake, yaweza kua mchanganyiko wa mboga za majani na vyakula vingine kama ilivyo salad hii.

(Kwa hisani ya: Tolly Kitchen)
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.