MAHASAMU SUDAN KUSINI WAKUBALI KUSITISHA VITARAIS wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wamefikia muafaka wa amani baada ya mgogoro uliodumu kwa miezi mitano.

Muafaka huo unataka kusimamisha mapigano mara moja na kuunda serikali ya mpito kabla ya kutengenezwa kwa katiba mpya na kufanyika kwa uchaguzi.

Mgogoro huo umegharimu maisha ya maelfu ya watu na zaidi ya milioni moja kukosa makazi.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, John Kerry, ambaye alifanya juhudi kubwa kuzileta pamoja pande mbili za mgogoro amesema kuwa muafaka huo ni ishara nzuri kwa mustakblai wa Sudan Kusini.

Kerry amesema kuwa safari ngumu na ndefu katika taifa hilo inaanza sasa na inapaswa kuendelea, akiongeza kuwa watu wa Sudan Kusini wameteseka kwa muda mrefu.

Umoja wa Mataifa umezituhumu pande mbili zinazohusika na mgogoro huo kwa kufanya uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji ya halaiki na magenge ya ubakaji.

Mahasimu hao wamesaini makubaliano hayo mjini Addis Ababa, Ethiopia jana, baada ya mkutano wao wa kwanza wa ana kwa ana kuanza.

Taarifa zinasema kuwa muafaka huo unatoa wito wa kusimamisha mapigano ndani ya saa 24 baada ya kusainiwa na kisha makubaliano ya kudumu yatasainiwa.

Kiir na Machar walitarajiwa kutoa maagizo mara moja kwa vikosi vyao kuacha mapigano na kuruhusu usambazaji wa misaada ya kiutu.


Haijawa wazi nani atakayeunda serikali hiyo ya mpito iliyoelezwa katika vifungu vya muafaka huo.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.