MAPOROMOKO YA ARDHI YATEKETEZA ZAIDI YA WATU 2100

Wanavijiji wa Afghanistan wakiwa wamekusanyika kwenye eneo yalipotokea maporomoko ya ardhi katika wilaya ya Argo katika jimbo la Badakhshan, Mei 2, 2014.


Idadi ya watu waliokufa kutokana na maporomoko makubwa ya ardhi katika jimbo la Badakhshan kaskazini mashariki mwa Afghanistan imefikia zaidi ya watu 2,100, huku zoezi la kutafuta manusura likiendelea.

Msemaji wa gavana wa jimbo hilo amesema kuwa watu 2,100 kutoka katika familia 300 wamethibitishwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 4,000 wamekosa makazi kutokana na janga hilo.

Taarifa kutoka huko zinasema kuwa wanavijiji wameungana na vikosi vya polisi kuwatafuta manusura huku wakitumia zana duni.

Mamia ya makazi yameharibiwa vibaya sana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku kadhaa katika eneo hilo.

Eneo hilo limekuwa likikumbwa na matukio ya maporomoko ya ardhi katika miaka ya hivi karibuni.


Kwa mujibu wa mashirika ya misaada ya kimataifa, Afghanistan ni eneo lenye matukio mengi ya majanga ya asili, ambayo huathiri maisha ya maelfu ya watu kila mwaka.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.