MIJI MIKUBWA KUWEKEWA KAMERA ZA UCHUNGUZI

 

Katika kuchukua hatua za kukabiliana na uhalifu nchini, serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inakamilisha mazungumzo na baadhi ya makampuni ili kuweka kamera maalumu za ulinzi katika miji mbalimbali nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, aliliambia Bunge jana kuwa wizara yake ilikuwa ikifanya mazungumzo na makampuni makubwa kuhusu suala hilo na kwamba hivi karibuni kamera hizo za CCTV zitaanza kutumika.

Alisema hatua hizo zinachukuliwa kufuatia ongezeko la matukio ya uhalifu katika miji mikubwa kama vile Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Zanzibar. “Tunafanya mazungumzo na makampuni madhubuti kuhusu mfumo wa uchunguzi… tunatarajia kuanza kutekeleza mradi huu muda si mrefu,” alisema Waziri  Chikawe.

Alisema tahthmini ya awali imeshafanyika katika miji ya Dar es Salaam na  Zanzibar na kwamba utekelezaji utaaza hivi karibuni.

Kwa mujibu wa waziri huyo, baada ya kuweka mfumo huo Dar es Salaam na  Zanzibar, mradi huo utaendelea kwenye miji mingine mikubwa nchini.

“Hili ni suala la kawaida kwa malengo ya ulinzi… tutaanza na Dar es Salaam na Zanzibar na baadaye tutaelekea kwenye maeneo mengine,” alisema.

Waziri Chikawe alikuwa akimjibu mbunge wa Mwibara (CCM) mheshimiwa Kangi Lugola aliyetaka kujua ni lini serikali itaweka kamera za CCTV katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Tanga, Moshi, Morogoro, Mbeya na Arusha. Mheshimiwa  Kangi Lugola alieleza kuwa miji hiyo imekuwa na matukio mengi ya uhalifu na kwamba kuna haja kwa serikali kutumia teknolojia ya kisasa kukabiliana na hali hiyo.

Aidha, bwana Lugola alipingana na serikali kuruhusu makampuni binafsi kuweka kamera za CCTV, akisema masuala yanayohusu usalama wa taifa yanatakiwa kupewa kipaumbele.

“Tumebinafsisha kila kitu; makampuni, mshamba na mali nyingine nyingi za umma… leo tunazungumzia makapuni binafsi kuweka kamera za CCTV… serikali inatakiwa kuwa makini jinsi inavyolishughulikia suala hili,” alisema.

Hata hivyo, waziri Chikawe alisema kuwa serikali iko makini na imejizatiti kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

Akizungumzia hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ajali za barabarani, naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Pereira Silima alisema kuwa serikali inakamilisha mpango wa kuweka mfumo maalumu wa kufuatilia magari.


CHANZO: The Citizen
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.