MILIPUKO YA MABOMU YAUA KADHAA

Police work to control a crowd of onlookers at the scene of an explosion on May 16, 2014 on the outskirts of Nairobi
Polisi wakijaribu kuudhibiti umati wa watu kwenye eneo la tukio la milipuko ya mabomu iliyogharimu maisha ya watu 10 Mei 16, 2014.Kwa uchache watu 10 wamepoteza maisha na zaidi ya 70 kujeruhiwa baada ya kutokea milipuko miwili kwenye soko la Gikomba mjini Nairobi.

Polisi wanasema kuwa mlipuko mmoja ulipiga gari moja ya abiria aina ya daladala, huku bomu la pili likilipuka ndani ya soko hilo.
Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa jiji la Nairobi, Benson Kibue, mtuhumiwa mmoja amekamatwa kuhusiana na shambulizi hilo.

Naye msemaji wa Hospitali Kuu ya Kenyatta National Hospital, Simon Ithae,  amesema kuwa kwa uchache watu 70 wamejeruhiwa katika tukio hilo, wengi wao wako katika hali mbaya,

Miji ya Nairobi na Mombasa imekuwa ikikumbwa na mfululizo wa milipuko tangu Septemba mwaka jana.

Mnamo Aprili 13, watu wanne, wakiwemo polisi wawili, walipoteza maisha katika mlipuko wa bomu lililotegwa kwenye gari nje ya kituo kimoja cha polisi mjini Nairobi.

Mwezi Septemba mwaka jana, shambulizi lililofanywa kwenye jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi liliwaua watu wasiopungua 67.

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabab kutoka Somalia wamekuwa wakitupiwa lawama za mashambulizi hayo.


Wanamgambo hao walisema kuwa shambulizi la westgate ni radiamali dhidi ya uwepo wa jeshi la Kenya nchini Somalia. Askari wa Kenya pamoja na wengine kutoka nchi za Unagda Burundi, Djibouti, Sierra Leone na Ethiopia ni sehemu ya Kikosi cha Umoja wa Afrika nchini humo (AMISOM).
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.