PICHA MBALI MBALI KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA

  Mbunge wa kuteuliwa Mhe.James Mbatia akifurahia jambo na Mhe.Shyrose Banji Mbunge wa Afrika Bunge la Afrika ya Mashariki.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta akijibu hoja za wabunge kabla Bunge halijapitisha Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa Mwaka 2014/2015.

Maofisa wa wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki wakiwa pamoja na Wabunge wa Afrika ya Mashariki wakifuatilia kikao cha Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa 
Mwaka 2014/2015.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Joyce Mapunjo mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2014/2015.

Mbunge wa Chalinze,Mhe.Ridhiwani Kikwete (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki,Mhe. Shyrose Banji 

 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe.Samweli Sitta na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ,Joyce Mapunjo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Maofisa wa wizara yake pamoja na Wabunge wa Afrika ya Mashariki mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kwa Mwaka 2014/2015.
Picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii.Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.