PICHA YA POLISI ALIYEIKANYAGA ENEO TAKATIFU YAZUSHA GHADHABU DUNIANI

Kaaba, ambayo ipo katika msikiti mtukufu wa Makkah ndio eneo takatifu linaloheshimiwa zaidi na waumini wa dini ya Kiislamu ulimwenguni.


Picha ya polisi mmoja akiwa ameegemea kwenye eneo Tukufu la Kaaba mjini Makkah nchini Saudi Arabia huku akiwa amelikanyaga kwa kiatu chake imezua sokomoko kwenye vyombo vya habari katika ulimwengu wa Kiislamu.

Gavana wa mji wa Makkah, Mwanamfalme Mishal Bin Abdullah Bin Abdul Aziz, ameamuru uchunguzi ufanyike juu ya tukio hilo, akisema kuwa kitendo hicho hakiwezi kuvumiliwa.

Aidha Mwanamfalme Mishal ametaka hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya polisi huyo kwa kushindwa kutambua heshima aliyopewa ya kutoa huduma katika eneo hilo tukufu zaidi kwa waumini wa dini ya Kiislamu duniani.

Magazeti nchini Saudi Arabia yalichapisha habari hiyo yakielezea kushtushwa na tukio hilo, huku mitandao ya kijamii ikizua maoni anuai juu ya picha hiyo.

Katika utamaduni wa Waarabu ni tusi kubwa kumuonesha mtu kikanyagio cha kiatu au kumtupia kiatu au kukikanyaga kitu kitukufu au mtu ukiwa hujavua kiatu.


Kaaba, ambayo ipo katika msikiti mtukufu wa Makkah ndio eneo takatifu linaloheshimiwa zaidi na waumini wa dini ya Kiislamu ulimwenguni.

CHANZO: Al-Arabiya
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.