PROFESA ANA TIBAIJUKA ATOWA ZAWADI YAKE YA TSH.9,500,000 KWA MAMA SHUJAA WA CHAKULA

Mgeni Rasmi Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akimkabidhi zawadi ya Tsh 5,000,000 Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga kutoka Nansio Ukerewe Mwanza.

Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 Bahati Muriga kutoka Nansio Ukerewe Mwanza akionesha zawadi yake ya Tsh 5,000,000 aliyokabidhiwa na Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka.

 Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akimkabidhi David Sevuri  zawadi ya Tsh 2,000,000 kwa ajili ya vijana wote walioshiriki katika shindano la Maisha Plus.

Mama Shujaa wa Chakula pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe ya  Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kukabidhi zawadi yake rasmi.

 Mkurugenzi mtendaji wa DMB ambao ndio wamiliki wa Shindano la Maisha Plus Masoud Ally 'Kipanya' akiwa anaendelea kuendesha ratiba wakati wa Sherehe fupi za Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kukabidhi zawadi kwa washindi wa Mama shujaa wa Chakula pamoja na washiriki wote wa Maisha Plus 2014.

 Mgeni Rasmi Waziri wa Nyumba Ardhi na maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka akitoa Hotuba yake fupi ya kuwapongeza washiriki wote katika shindano la kumsaka Mama Shujaa wa Chakula na mpaka kupatikana mshindi, pamoja na kuwapongeza pia aliwaomba wakawe mabalozi wazuri kwa kwenda kuwafundisha wakulima wengine kile ambacho wamejifunza.


Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.