RAIS OBAMA KATIKA ZIARA YA KUSHTUKIZA NCHINI AFGHANISTAN

 Obama

Rais wa Marekani Barack Obama ametua nchini Afghanistan kwa ziara ya kushtukiza kwa lengo la kuwapongeza askari wa Marekani ambao wamekuwa nchini humo kwa vita vya muda mrefu zaidi kuwahi kupiganwa na Marekani.

Obama aliondoka White House na kutua leo jioni kwenye uwanja wa jeshi la anga ulioko Bagram nje kidogo ya mji wa Kabul.

Katika ziara hiyo fupi Obama anatarajia kukutana na makamanda wa jeshi la Marekani na viongozi wa kiraia nchini Afghanistan, lakini haijawekwa wazi iwapo atakutana na Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai au yeyote katika wagombe wanaowania kiti cha urais wa nchi hiyo.


Safari hiyo, ambayo haikutangazwa awali kwa sababu za kiusalama, imekuja huku Marekani ikijiandaa kuadhimisha siku ya mashujaa ambapo huwatunuku wapiganaji wake waliokufa vitani au waliowahi kupigana vita.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.