TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA MOI.

      Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) 
    Bw.Jumaa Almasi (katikati)akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hatua iliyofikiwa katika             kupanua  huduma za Taasisi hiyo ikiwemo kukamilika kwa jengo jipya la kisasa litakalokuwa na vifaa vya kisasa      kama MRI (magnetic Resonance Imaging) CT-SCAN (Computerized Tomography).kushoto ni Afisa Habari wa Idara    ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum na kulia ni Afisa uhusiano wa Taasisi hiyo Bw. Patrick Mvungi.Muonekano wa Jengo jipya la Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) ambalo linatarajiwa kukamilika mapema mwaka huu,kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia Taasisi hiyo kupanua huduma zake na kupunguza idadi ya wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje ya nchi kwa kwa asilimia 80 ikiwa ni juhudi za Serikali kuboresha huduma za Afya hapa nchini.
(Picha zote na Idara ya Habari Maelezo)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dar es Salaam, 26/05/2014 Mradi wa jengo jipya la MOI, (MOI Phase III) ambao utagharimu zaidi ya Tshs billion 30 utaisaidia serikali kupunguza gharama za rufaa za kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi kufuata huduma kutokana na  baadhi ya huduma na vipimo kutokuwepo nchini,rufaa hizo huwa  ni za gharama kubwa sana
Mradi huo utaiwezesha MOI Kuwa na vifaa vya kisasa vya MRI (Magnetic Resonance Imaging), CT-SCAN (Computerized Tomography) ambavyo vichache sana hapa nchini na Cyberknife digital angiography (DSA) ambacho hakipo kabisa Tanzania
 MOI itaweza kuwa na vitanda 20 vya wagonjwa mahututi kutoka 8 vilivyopo sasa,wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (high dependence ward ) vitanda 24 ambayo haipo kwa sasa,wodi ya wagonjwa wa kuchangia huduma (cost sharing) zikiwa na jumla ya vitanda 240 na wodi za wogonjwa wa kulipia 62 na kuifanya taasisi kuwa na vitanda 380 kutoka 159 vilivyopo na hivyo kuondokana na adha ya wagonjwa kurundikana wodini na kulala kwenye magodoro chini
Aidha,mradi utatoa fursa ya Ajira 243 kwa watanzania katika kada za udaktari,uuguzi,wauguzi wasaidizi na kada nyingine ambazo zimeainishwa kutokana na mahitaji
Huduma nyingine ni uanzishwaji wa mfumo “paperless system” ambao unahusisha utoaji wa huduma kwa kutumia mfumo wa kieletroniki zaidi na kuachana na mfumo wa sasa wa kutumia Mafaili ya makaratasi mengi na unafanya wagonjwa watumie muda mwingi kabla ya kupata huduma
Taasisi ya MOI inawaasa watanzania kuachana na kasumba ya kukimbilia kupata matibabu nje ya nchi kwa magonjwa yanayoweza kutibika hapa nchini ambapo wanatumia gharama kubwa wakati huduma hizo zinapatikana hapa nchini kwa gharama nafuu  
-XXX-
IMETOLEWA NA
MKURUGENZI MTENDAJI

TAASISI YA TIBA YA MIFUPA MOI
Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.