UMOJA WA MATAIFA WAIWEKA BOKO HARAM KATIKA MAKUNDI YA UGAIDI

Boko Haram Takfiri militants (file photo)
Wapiganaji wa kundi la Boko HaramUmoja wa Mataifa umeliorodhesha kundi la waasi wa Nigeria la Boko Haram kuwa katika makundi ya kigaidi kwa kitendo chake cha kuwateka wasichana wapatao 300 nchini humo na kulihusisha moja kwa moja na mtandao wa Al-Qaeda.

Kamati ya Vikwazo ya Baraza la Usalama dhidi ya kundi la al-Qaida imechukua hatua hiyo katika kikao chake kilichofanyika hapo jana.

Uamuzi wa kamati hiyo umeiwekea Boko Haram vikwazo vya silaha na kuzishikilia mali zake.

Balozi wa Canada kwenye Umoja huo na ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Vikwazo dhidi ya al-Qaida, Gary Quinlan, amesema kuwa kamati yake imeenda mbali zaidi kwa kuhakikisha kuwa kila atakayelisaidia kundi hilo kwa zana au fedha naye atawekwa katika orodha ya vikwazo hivyo.

Hata hivyo, ofisa huyo amebainisha kuwa hatua hiyo inaweza isiwe na athari ya haraka kwa kundi hilo ingawa anaamini kuwa ni hatua muhimu inayolenga kuziba mifereji ya misaada kwa kundi hilo.

Wakati huohuo, jana waandamanaji walifanya maandamano kuelekea kwenye makazi ya Rais Goodluck Jonathan mjini Abuja kuelezea hasira zao kutokana na  serikali kushindwa kuwaokoa wasichana hao waliotekwa. Walimkosoa rais huyo kwa madai ya kutokuwa na uchungu na kwa hatua yake ya kukataa kukutana nao.


Shule nyingi nchini humo zilifungwa kulaani uhalifu wa kundi la Boko Haram ambalo mara nyingi limekuwa likidai kuhusika na mashambulizi kadhaa katika maeneo mbalimbali ya Nigeria tangu mwaka 2009.


Kwa zaidi ya miaka minne sasa, ghasia katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo zimegharimu maisha ya watu 3,600, yakiwemo mauaji yanayodaiwa kufanywa na vikosi vya usalama.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.