UTALII WETU TANZANIA, SIMBA 11 WASHINDWA KUMLA NYATI DUME.

Ilikuwa ni vita ambayo haikuruhusu mtoto kutumwa maji dukani.

                   Kundi la Simba likielekea katika mawindo yake baada ya kuona kundio la Nyati.                                     Tukio hili lilijiri hivi karibuni katika Hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania.
Nyati huyu ndio aliingia katika mtego na kuanza kufukuzwa na Simba. Kwa Mbali gari la Watalii likija eneo hilo na baada ya muda magari 12 yaliyo na watalii mbalimbali yalifika katika eneo hilo na kushuhudia mtanange mkali kati ya Simba na Nyati. Mpigapicha wa Gazeti la Uengereza la Daily Mail, Scott Macleod alinasa taswura hizi.
Watalii walikata kiu yao vya kutosha maana moja ya vitu vinavyowavutia watalii ni kumuona Simba au Chui akiwa mawandoni. Lakini hakika kwa Hifadhi za Tanzania hili linawezekana na watalii karibuni mjionee haya.
Watalii waliongezeka na kushuhudia  jitihada za Simba walau kumuangusha Nyati hiyo lakini biola mafanikio.
 Watalii wakifurahia kivutio hicho ndani ya ardhi ya Tanzania.   Simba hawakuhofua macho wala mingurumo ya magari iliyokuwa imewazunguka mahali hapo wakati vita yao ya kumla Nyati ikiendelea. 

           Hakika Nyati ni The Big 5 Animal. Licha ya Simba kuwa wengi lakini walishindwa                 kumuangusha Nyati huyu na kujipatia kitoweo. Simba walitawanyika kwenda kutafuta                                                                       nguvu zaidi.
Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.