VENEZUELA KUPELEKA SHEHENA YA MAFUTA PALESTINAVenezuela inatarajia kutuma mafuta ya mazito kwenda Palestina kama sehemu ya mkataba wake na Mamlaka ya Palestina ili kuwapa ahueni Wapalestina dhidi ya mateso ya vikwazo vya Israeli.

Rais wa Mpito wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesaini makubaliano ya nishati na Rais wa Venezuela Nicolas Maduro katika mji mkuu wa nchi hiyo,  Caracas.

“Ahsante Venezuela kwa kuiunga mkono Palestina, ahsante Venezuela kwa kusaidia kuvunja ukiritimba unaofanywa na Israel dhidi ya uchumi wetu,” alisema Abbas baada ya kusaini mkataba huo.

Rais Maduro alisema kuwa mkataba huo wa nishati “ni kutoka Venezuela kwenda  Palestina kwa ajili ya kuipatia mafuta mazito inayoyahitaji kwa ajili ya kukuza na kuendeleza uchumi wake. Mkataba huu ni kwa ajili ya kujenga umoja na ushirikiano kati ya Venezuela na Palestina.”

Aidha, pande hizo mbili zilijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mgogoro baina ya Israeli na Palestina.

Abbas amekuwa katika ziara ya siku mbili nchini Venezuela kwa lengo la kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya pande mbili.

Anapanga kutoa wito wa kuliunga mkono ombi la Mamlaka ya Palestina kupewa hadhi ya kuwa mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Nchi za Amerika ya Kusini (UNASUR), Jumuiya ya Mataifa ya Amerika ya Kusini na Caribbean (CELAC) na Jumuiya nyingine za Ukanda huo.

Mwezi Novemba mwaka 2012 Mamlaka ya Palestina ilipata hadhi ya kuwa mwanachama mwangalizi katika Umoja wa Mataifa licha ya upinzani mkali kutoka Israeli na Marekani.

Ziara hiyo imekuja baada ya vyama vya Hamas, PLO na Fatah kuondoa tofauti zao na kuunda serikali ya pamoja
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.