WAHAMIAJI HARAMU 17 WAKAMATWA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE  21.05.2014.
  • JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI KATIKA MATUKIO TOFAUTI.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA   KWA KUKUTWA NA POMBE KALI
  • WAHAMIAJI HARAMU 17 WAKAMATWA KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI
KATIKA MISAKO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA  KUTOKANA NA MISAKO MBALIMBALI ILIYOFANYIKA.  KATIKA TUKIO HILO   JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA OSCAR S/O MBELEWA,[36],MKAZI WA KAFUNDO- IPINDA MKAZI WA KIJIJI CHA MAZIMBO  KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI KG 72 KWENYE GUNIA AKIWA NA PIKIPIKI YAKE YENYE NO T.477 CMZ AINA YA  SANLG.   TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 20.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO KATIKA KITONGOJI STAMICO, KIJIJI NA KATA YA MKOLA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.
AIDHA; JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA CASIAN S/O JOSEPH, [19], MKAZI WA UBARUKU AKIWA NA BHANGI KETE 65, SAWA NA UZITO WA GRAM 325. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 20.05.2014 MAJIRA YA SAA 17:00HRS KATIKA KIJIJI NA KATA YA UBARUKU, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
VILEVILE; JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA HASSAN S/O ISMAIL, [30], MKAZI WA MBUGANI  AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU AINA YA  BOSS KATONI MOJA [01]. TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 20.05.2014 MAJIRA YA SAA 11:25HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA LUKUYU, KATA YA MWAYA, TARAFA YA NTEMBELA, WILAYA YA  KYELA,   MKOA WA MBEYA, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA BHANGI/POMBE HARAMUZILIZOPIGWA MARUFUKU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA  NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA NYABEDA S/O SAMSON, [32] RAIA NA MKAZI WA NCHINI BURUNDI PAMOJA NA WENZAKE 16 WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI. AIDHA ALIKAMATWA MTANZANIA HAMIS S/O MWAKALINGA [29] MKAZI WA SOWETO AKIWA ANAWASAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU HAO. TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO TAREHE 20.05.2014 MAJIRA YA SAA 01:00HRS HUKO MWANJELWA STENDI YA TUKUYU, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI. PAMOJA NA KUMFISHA MAHAKAMANI MTUHUMIWA HAMISA MWAKALINGA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI  ANATOA WITO KWA JAMII PINDI WANAPOWAONA/KUWATILIA MASHAKA WATU WASIOWAHAMU KUTOA TAARIFA KWENYE VYOMBO HUSIKA ILI WAKAMATWE NA KUHOJIWA.
Signed by:
 [ AHMED Z. MSANGI – SACP ].
 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.