ANGALIA PICHA ZA CHATU MUUWA WATU ARUSHA, SASA KAUWAWA.

Wiki chache zilizopita wakazi wa Kinondoni walimuua Mamba ambaye alikua akiishi karibu na bwawa maeneo hayo ya Kinondoni, block 41 walichoshwa nae wakaamua kumuua,sasa baada ya mamba hapa kuna stori ya Chatu aliyeuwawa Arusha.
Kwa mujibu wa Arusha yetu Blog wanasema kuwa Chatu huyo aliuwawa na wananchi, Chatu ambaye alionekana maeneo ya Sakina Arusha na akiwa amefungwa kitambaa chenye maaandishi mekundu.
Wakazi wa eneo la Sakina wamepatwa na mshtuko mkubwa, kikubwa zaidi kwa Chatu huyo ni kuwa inasemekana alitokea ndani aliuwawa na Wananchi baada ya kuonekana.
Mara baada ya kuonekana kwa Chatu huyo wananchi walijipanga kisha wakafanikiwa kumuua ingawa kulitokea utata baada ya Mama mwenye nyumba aliyetokea Chatu huyo akipinga kutokuuliwa kwa Chatu huyo,Chatu huyo aliuwawa kisha akakatwa vipande vipande .
  
Nihatari kubwa tuwe makini
Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.