MSIBA MZITO KWA CHADEMA NA TAIFA LA TANZANIA.

Marehem Shida Salum (Mama yake Zitto Kabwe)
 Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, mchana huu amefiwa na mama yake mzazi aliyeugua kwa muda mrefu.
Bi Shida Salum, amefariki katika hospitali ya AMI jijini Dar Es Salaam ambako amekuwa akitibiwa kwa zaidi ya wiki mbili.
Awali Bi Shida alikuwa amepelekwa India kwa ajili ya matibabu kabla ya kurejeshwa nchini.
Zitto ni mbunge kijana kutoka CHADEMA, ambaye amepata umaarufu mkubwa kutokana na uhodari wake wa kujenga hoja.
Mama yake wakati wa uhai alikuwa mshiriki katika maswala ya kisiasa, ambapo alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Mzizima24 tunatoa pole kwa Zitto Kabwe, familia na wote walioguswa na msiba huu.
Tutawaletea habari zaidi zitakavyopatikana.
                                      Marehem Shida Salum (Mama yake Zitto Kabwe)
               
Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.