MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA FIMBO KICHWANI WAKICHEZA NGOMA ZA JADI

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 03.06.2014.
  • MTU MMOJA AFARIKI DUNIA AKIWA ANAPATIWA MATIBABU BAADA YA KUPIGWA FIMBO KICHWANI WAKIWA WANACHEZA NGOMA ZA JADI.
  • WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE SABA KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
  • WATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUAWA NA MMOJA KUKAMATWA KATIKA JARIBIO LA UNYANG’ANYI.
  • JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA SILAHA/BUNDUKI AINA YA GOBOLE.
 KATIKA TUKIO LA KWANZA:
 MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA NDONYA SUGU (23) MKAZI WA KIJIJI CHA MAFYEKO ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA MATIBABU KATIKA ZAHANATI YA CHA BITIMANYANGA BAADA YA KUPIGWA FIMBO KICHWANI.
 TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.06.2014 MAJIRA YA SAA 02:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA ITAGA, KIJIJI CHA BITIMANYANGA, KATA YA MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MAREHEMU ALIPIGWA FIMBO KICHWANI TAREHE 01.06.2014 MAJIRA YA SAA 16:30 JIONI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SHAGEMBE KUNAWIJI (54) MKAZI WA KIJIJI CHA BITIMANYANGA WAKATI WANACHEZA NGOMA ZA KABILA LA KISUKUMA MAARUFU KWA JINA LA CHAGULAGA KIJIJINI HAPO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
 KATIKA TUKIO LA PILI:
WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.163 ATQ AINA YA TOYOTA HAICE LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA GODFREY AWDHI NGOLE (32) MKAZI WA IGURUSI KUACHA NJIA NA KISHA KUPINDUKA KATIKA ENEO LA MAMBI WILAYA YA MBARALI.
ABIRIA MMOJA KATI YA WAWILI ALITAMBULIKA KWA JINA LA ELIZABETH MKARAWE (30) MKAZI WA IGURUSI NA 2. MSICHANA MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI WALIFARIKI DUNIA. AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 02.06.2014 MAJIRA YA SAA 11:50 ASUBUHI KATIKA ENEO LA MAMBI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/NJOMBE.
AIDHA KATIKA TUKIO HILO WATU SABA WALIJERUHIWA KATI YAO WANAUME WATATU NA WANAWAKE WAWILI AKIWEMO DEREVA WA GARI HILO.CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MIILI YA MAREHEMU NA MAJERUHI WAPO HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WA NAKONDE NCHINI ZAMBIA LINAMSHIKILIA JAMBAZI MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JIMMY NYILENDA RAIA WA ZAMBIA BAADA YA  KUJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI KATIKA JARIBIO LA UNYANG’ANYI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.06.2014 MAJIRA YA SAA 17:45 JIONI KATIKA ENEO LA MPAKANI KATI YA TANZANIA NA ZAMBIA [TUNDUMA/NAKONDE]. INADAIWA KUWA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIFYATUA RISASI OVYO KWA LENGO LA KUWAPORA PESA WABADILISHAJI FEDHA WA ENEO HILO NA POLISI WA TUNDUMA [TANZANIA] NA NAKONDE [ZAMBIA] WALIKABILIANA NA MAJAMBAZI HAO. KATIKA MAJIBIZANO HAYO, MAJAMBAZI WATATU WALIUAWA WAWILI  WAKIFAHAMIKA KUWA NI SIKAPWITE BONIPHACE  MFANYAKAZI WA COUNCIL NAKONDE RAIA WA ZAMBIA NA CHAPWA KIPAKWA RAIA NA MKAZI WA ZAMBIA  NA MWINGINE HAKUWEZA KUFAHAMIKA.
AIDHA MAJAMBAZI WENGINE WALIWEZA KUKIMBIA NA JAMBAZI MMOJA JIMMY NYILENDA RAIA WA ZAMBIA AMEKAMATWA AKIWA  MAHUTUTI BAADA YA  KUJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI.

KATIKA TUKIO HILO SILAHA MBILI AINA YA AK-47 ZENYE NAMBA 625562 NA 1963EC58 ZILIKAMATWA. HATA HIVYO KATIKA MAJIBIZANO HAYO RAIA WAWILI WA NAKONDE –ZAMBIA WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA.HAKUNA MADHARA KWA ASKARI NA SILAHA ZIPO POLISI NAKONDE ZAMBIA. JUHUDI ZA KUWATAFUTA MAJAMBAZI WALIOKIMBIA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATUHUMIWA HAO WA TUKIO LA UJAMBAZI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUWA MAKINI KWA KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA KAZI ZAO.
KATIKA MSAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI WANYAMAPORI TANAPA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AMOS NAIMWA (30) MKAZI WA KIJIJI CHA UTURO AKIWA NA SILAHA/BUNDUKI MOJA AINA YA GOBOLE NA GOROLI 12 BILA KIBALI.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 31.05.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA KATIKA KIJIJI NA KATA YA   ULANGA, TARAFA YA   RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUWINDAJI HARAMU, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARTIBU ZA UMILIKAJI SILAHA KIHALALI  ILI KUEPUKA MATATIZO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Share on Google Plus

About Mr. Lulela

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.