CHELSEA, YAIPIGA 3-1 LEICESTER, SHEREHE RASMI ZA UBINGWA JUMAPILI DARAJANI

BADO pointi tatu Chelsea kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu. Hiyo inafuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Lecester City Uwanja wa King Power usiku wa kuamkia leo. 
Ushindi huo umeifanya Chelsea ya kocha Mreno Jose Mourinho ifikishe pointi 80 baada ya kucheza mechi 34, mbele ya mabingwa watetezi Manchester City pointi 67 za mechi 34, Arsenal pointi 67 mechi 33 na Manchester United pointi 65 mechi 34. 
Marc Albrighton alianza kuifungia Leicester dakika ya 54, kabla ya Didier Drogba kuisawazishia Chelsea dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili.  John Terry akaifungia Chelsea zimesalia dakika 11 na Ramires akamalizia la tatu dakika ya 83.
Chelsea inaweza kutangaza ubingwa Jumapili katika mechi na Crystal Palace Uwanja wa Stamford Bridge.
Kikosi cha Leicester kilikuwa; Schmeichel, Wasilewski, Huth/De Laet dk24, Morgan, Albrighton, King/James dk18, Drinkwater, Cambiasso, Konchesky, Ulloa na Vardy/Mahrez dk77.
Chelsea; Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian/Zouma dk84, Fabregas/Mikel dk90, Hazard/Cuadrado dk88 na Drogba.
Didier Drogba (centre) was the star of the show for Chelsea - and he was leading his team-mates in celebrations at full time
Didier Drogba (katikati) akishangilia na wenzake jana
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.