DORTMUNG YAITOA BAYERN KOMBE LA UJERUMANI KWA MATUTA, YATINGA FAINALI

Bayern Munich wameng’olewa kwenye michuano ya Kombe la Ujerumani na wapinzani wao wakubwa Borussia Dortmund ambao sasa wametinga fainali.


Bayern wameng’olewa kwa penalti 3-2 huku Xabi Alonso, Phillip Rahm wakikosa baada ya kuteleza. Dortmund walikuwa ugenini jijini Munich.

Halafu kipa nyota, Emmanuel Neuer ambaye aliokoa penalti moja, naye akakosa na Dortmund ikasonga.

Dakika 90 za mechi hiyo ziliisha kwa sare ya bao 1-1, Dortmund wakisawazisha kupitia Aubameyang baada ya Robert Lewandowski kufunga la kuongoza kwa Bayern.
 Sasa Dortmund inasubiri mshindi kati ya Werder Bremen dhidi ya Arminia ambaye atacheza naye fainali.Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.