ETOILE WAIFANYIA YANGA KIKAO KIZITO TUNISIA...

 Etoile du Sahel wamefanya kikao kizito kuhakikisha wanaing’oa Yanga.


Kikao hicho kimejumuisha wachezaji wakongwe wa zamani wa timu hiyo, wakuu wa makundi ya mashabiki pamoja na viongozi wa zamani.
 
Kikao hicho kimefanyika makao makuu ya klabu hiyo mjini Sousse, Tunisia na imeelezwa hoja nyingine ilikuwa ni kujadili suala la Ligi Kuu ya Tunisia pamoja na masuala mengi ya uchaguzi.

Ingawa mengi yaliyozungumziwa yamefanywa ni siri na kutajwa machache, imeelezwa Yanga ilikuwa ni sehemu ya ajenda kuu.
 
Baadhi ya wajumbe walionya Etoile kuhakikisha hawaidharau Yanga hata kidogo na ikiwezekana wajiandaa utafikiri walipoteza mechi jijini Dar.

Yanga na Etoile zilitoka sare ya bao 1-1 jijini Dar, hivyo Yanga inatakiwa kushinda au sare ya kuanzia bao 2-2 ili isonge mbele katika mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho.

Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.