RAIS KIKWETE AKUTANA NA RAIS MSTAAFU WA MAREKANI BILL CLINTON JIJINI DAR ES SALAAM APRIL 28, 2015.

01
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.na kisha kufanya mazungumzo na rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini  kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiriwa na taasisi za Clinto Development Initiative (CDI) na Clinto Health Access Initiative (CHAI).
2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam leo April 28, 2015.rais huyo wa 42 wa Marekani yuko nchini  kukagua miradi ya maendeleo na afya inayofadhiriwa na taasisi za Clinto Development Initiative (CDI) na Clinto Health Access Initiative (CHAI).PICHA NA IKULU
---------------------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Aprili 28, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa 42 wa Marekani, Mheshimiwa Bill Clinton ambaye anafanya ziara nchini. 
Baada ya mazungumzo hayo, viongozi hao walipata chakula cha mchana cha pamoja kabla ya kiongozi huyo wa Marekani kuondoka Ikulu, Dar es Salaam.
 Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wawili walizungumzia baadhi ya miradi ambayo inadhaminiwa na kugharimiwa na Taasisi ya Clinton Foundation katika nyanja ya afya na hasa katika maeneo ya utoaji wa dawa za kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, afya za akina mama na jinsi ya kupunguza vifo vya watoto wadogo chini ya miaka mitano na jitihada za kupambana na malaria, Nyanja ya kilimo hasa uzalishaji wa mbegu kwa wingi na kilimo cha soya.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

28 Aprili,2014
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.