Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa akutana na Viongozi wa Elimu nchini Singapore

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa pamoja na viongozi wa elimu nchini watembelea Singapore kujifunza jinsi nchi hiyo ilivyofanya mageuzi makubwa katika mfumo wa elimu na mafunzo. 
Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, unalenga kuendeleza wanafunzi katika kuwapatia stadi muhimu zinazohitajika kwa maendeleo ya nchi. 
Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, umeweka mkazo zaidi katika kutoa mafunzo ya ufundi stadi ambayo yanatoa ujuzi kwa mhitimu kuweza kufanya kazi katika kada ya kati. 
Takwimu za elimu zinaonyesha kuwa, asilimia 29.4 ya wahitimu wanajiunga na vyuo vikuu; asilimia 28.2 wanajiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na asilimia 46.4 wanajiunga na vyuo vya utaalamu mbalimbali (Polytechnic). 
Katika ziara hiyo Dkt Kawambwa na ujumbe wake walipata nafasi ya kutembelea chuo kikuu cha Taifa cha Singapore (National University of Singapore), Chuo cha Elimu ya Ufundi (Institute of Technical Education) na Chuo cha Ufundi stadi (Republic Polytechnic) ambapo katika vyuo hivyo walipata nafasi ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi pamoja na walimu.
Waziri wa Elimu na ujumbe wake wakiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Chuo kikuu cha Taifa Singapore. Ujumbe wa Tanzania ulitembelea chuo hicho ili kujionea na kujifunza ambavyo elimu ya ngazi ya chuo kikuu inavyotolewa nchini Singapore
Viongozi wa wizara ya Elimu na Mafunzo kutoka Tanzania na Viongozi wa Elimu wa Singapore wakiwa katika mkutano wa pamoja katika kubadilisha mbinu na mikakati mbalimbali ambayo inaweza kuboresha na kuleta mageuzi katika mifumo ya elimu wa nchi hizi mbili
 Waziri wa Elimu na Mafunzo Dkt Shukuru Kawambwa akielezea Jambo katika Mkutano kati ya viongozi wa elimu kutoka wa Tanzania na Viongozi wa Wizara ya Elimu ya nchini Singapore. 
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.