MAYWEATHER AMSHINDA KWA POINTI PACQUIAO

RAUNDI KWA RAUNDI 
Mayweather Raundi Pacquiao 
          101        9
           92       10
           93       10
           9       10
          105        9
           9       10
          10        9
          108        9
          109       10
           910       10
          1011         9
          1012        10
         115JUMLA       115
BONDIA Floyd Mayweather amekamilisha pambano lake la 49 bila kupoteza, baada ya kumshinda kwa pointi Mfilipino, Manny Pacquiao.
Katika pambano hilo lililofanyika ukumbi wa MGM Granc mjini Las Vegas, Mmarekani huyo ameshinda kwa pointi za majaji wote, 118-110, 116-112 na 116-112.
Tofauti na ilivyotarajiwa, Pacquiao hakuweza kurusha ngumi nyingi kutokana na mpinzani wake kuhama hama ulingoni.
Mayweather aliitumia vizuri staili yake ya kupigana kwenye kona na kufanikiwa kumtupia ngumi nyingi za kudonoa mpinzani wake kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Kufika raundi ya 11, tayari mwelekeo wa pambano ulianza kuonekana ‘Mtu Pesa’ atashinda- ingawa Man Pac alikuwa anashangiliwa zaidi ukumbini.
Mayweather alistahili ushindi na alionyesha yeye ni bondia bora wa kizazi cha sasa.
Mayweather made contact with a straight right - a weapon he kept deploying against Pacquiao

Mayweather akimrushia konde mpinzani wake Pacquiao katika pambano lao lililomalizika hivi karibuni
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.