MTOTO WA MIAKA 8 AKUTWA KWENYE BEGI LA SAFARI

 The silhouette of an Ivorian boy, shown by an X-ray scanner, being smuggled in a suitcase and discovered at Ceuta land border crossing office, May 8, 2015. (AFP photo)

Mtoto wa miaka minane amekutwa akiwa amepakiwa katika begi la nguo na kusafirishwa kinyemela kwenye mpaka wa Hispania na eneo la Afrika Kaskazini, polisi wa nchi hiyo wamesema.

Mtoto huyo aitwaye Abou kutoka Ivory Coast alegunduliwa baada ya polisi wa Ceuta, jirani na Morocco, kuweka begi hilo kwenye mashine ya kupimia na kugundua kivuli cha kitu kisichokuwa cha kawaida.

Baada ya kulifungua walimku walimkuta mtoto, akiwa katika hali mbaya.


Hali ya wasiwasi aliyokuwa nayo mbebaji wa begi hilo, mwanamke mwenye umri wa miaka 19 raia wa Morocco, iliwafanya polisi kumtilia shaka katika kivuko cha El Tarajal na hivyo kupelekea kulipima begi hilo kwenye mashine maalumu.  Alikamatwa na saa kadhaa baadaye baba wa mtoto huyo, raia wa Ivory Coast akakamatwa kwenye mpaka huo.

Kwa mujibu wa gazeti la Hispania la El Pais, mwanamke aliyebeba begi hilo alilipwa pesa na baba wa mtoto huyo ili kumfanyia kazi hiyo.

Baba wa mtoto huyo, ambaye pia anaitwa Abou, ameripotiwa kuishi katika visiwa vya Canary nchini Hispania na alitarajia mwanaye huyo aungane naye.


Kila mwaka, maelfu ya wahamiaji na wanaotafuta hifadhi, ambao wanakimbia matatizo mbalimbali katika nchi zao, hujaribu kuvuka kuptokea Morocco kwenye Hispania kupitia kwenye mlango bahari wenye ukubwa wa kilometa 15 wa Gibraltar.

Wahamiaji hao hutumia mitumbwi na boti zisizokuwa na usalama na kuifanya safari yao kuwa ngumu na ya mashaka.Kadhalika, maelfu ya wahamiaji hujaribu kuingia Hispania kupitia miji ya Ceuta na Melilla karibu na mpaka wa nchi hiyo na Morocco. Serikali ya Hispania imeweka uzio wenye urefu wa mita saba ili kuwazuia wahamiaji wasiingie katika eneo la nchi hiyo.

Wahamiaji wengine hujaribu kuvuka mpaka kwa kujificha ndani ya magari ya mizigo, kuogelea au kuvuka kwa majahazi kwenye pwani ya Morocco na kuingia Hispania.
Share on Google Plus

About Kabuga Kanyegeri

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.