RONALDO APIGA HAT-TRIC YA 29 AKIIMALIZA SEVILLA

MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefunga hat-trick yake ya 29 tangu aanze kuchezea Real Madrid katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Sevilla katika La Liga usiku huu.
Ushindi huo unaifanya Real ifikishe pointi 85 na kupunguza pengo la pointi inazozidiwa na Barcelona hadi kubaki mbili baada ya timu zote kucheza mechi 35.
Hii inakuwa mara ya kwanza timu ya Unai Emery inafungwa nyumbani baada ya mechi 35 na ni Ronaldo anayevunja rekodi ya timu hiyo kucheza mechi 15 bila kufungwa.
Ronaldo alifunga mabao hayo katika dakika za 36, 37 na 69 Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan, wakati mabao ya Bacca kwa penalti dakika ya 45 na Iborrs dakika ya 79. 
Cristiano Ronaldo led Real Madrid to victory and scored twice for his team in the first half of the game
Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid mabao yote katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Sevilla
Share on Google Plus

About Mahamoud Salum

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.